USHUHUDA WA MBINGUNI NA KUZIMU NYISAKI CHAULA
USHUHUDA WA MBINGUNI NA KUZIMU
NYISAKI CHAULA
UTANGULIZI:Ndugu yangu kuna shuhuda nyingi sana zinazoanguka duniani, lakini wachache wanaozingatia kwa vile watoaji si wa dini zao au si wa madhehebu yao wala hawajulikani makanisani.Sasa ninakuomba ewe msomaji, tafuta mahali pa utulivu, mwombe Mungu na kusoma ushuhuda huu ili upokee kile ambacho Bwana amekuletea leo. Msichana huyu hivi sasa ameolewa na Mwinjilistii Lemsy Mheni pale Uyole Mbeya kwa lengo la kukuzahuduma yao. Kabila lake ni Mkinga wa Makete,.Msichana huyu anapatikana Uyole njia panda ya Malawi, Zambia na Dar es Salaam pembeni mwa kituo cha mafuta ya magari pale Uyole, Bwana awatangulie katika usomaji.
SURA YA 1
KUITWA:
Ilikuwa ni mwezi wa 12/1991 tulipochaguliwa vijana 10 kuombea Mkutano wa Kiroho ambao ulikuwa ukifanyika pale Uyole. Siku moja baada ya maombi ya usiku, nilala pamoja na dada zangu. Siku hiyo.nilala usingizi mzito ambao sijapata kuona. Usiku nilishangaa kukuta usingizi umetoweka kabisa,.hivyo nikabaki nikiwa macho, ndipo nikasikia sauti ikiita Nyisaki nikasikia lakini sikuitikia, ikaita mara ya pili pia sikuitika. Hata mara ya tatu ndipo nikaitika kisha nikasikia ile sauti ikisema Nimekuchagua kuwa mtumishi wangu ndipo nikatambua kuwa ni sauti ya Bwana, nikasema Bwana mimi ni mtoto mdogo tena hata chuochochote sijaenda nitawezaje kuifanya kazi hiyo? Bwana akaniambia mkumbuke Yeremia mtumishi wangu nilimchagua angali bado mdogo (Yeremia1:5) basi nikaendelea kubishana na ile sauti hadi dada yangu mmoja aliamka na kusema Mshukuru Mungu kwa sababu amekuchagua wewe. Ndugu msomaji kumbuka kuwa sauti hiyo nilisikia nikiwa macho kabisa na wala haikuwa ndoto na baada ya kusikia sauti hiyo mara ya pili na ya kwanza niliamka na kuthibitisha kabisa kuwa wote niliokuwa nimelala nao bado wamelala. Na hata huyo dada yangu alisema Mshukuru Mungu kwa sababu amekuchagua wewe nilitambua kuwa ni Mungu ndiye aliyemuelimisha na kumfunulia jambo hili. Baada ya yote haya tukamshukuru Mungu na kulala. Kesho yake tarehe 30/12/1991 ndipo nilipoonyeshwa mambo makuu ya ajabu (Yeremia 33:3)
SURA YA 2
JEHANAMU SEHEMU YA KWANZA NA MANGOJEO YA WAFU:
Ikiwa tarehe 30/12/1191 tulipoamka tukaenda kwenye semina na baada ya ile semina tuliamua kwenda kumuona rafiki yetu aliyeokoka ambaye kwa muda ule alikuwa hajiwezi yaani alikuwa anaumwa. Tulipofika pale nyumbani tukafungua ibada kwa maombi kisha tukaanza kujifunza jinsi Biblia inavyosema kwa njia ya maswali. Hata baada ya hapo tukaamua kufunga Ibada kwa maombi kama tukivyofungua. Tufunge kwa maombi na kumkabidhi ndugu yetu mikononi mwa Bwana, maana tulianza ibada yetu kwa kumshukuru Mungu kwa kuwa ndugu yetualikuwa hajambo.Ninachokumbuka ni kwamba tuliimba pambio moja ya kuabudu lakini sikumbuki kwamba tuliingia kwenye maombi au la tulipokuwa tunaimba ile pambio ya kuabudu, nikashangaa kuona kuwa nimechukuliwa niko sehemu tofauti kabisa na mazingira ya nyumbani.Ukiniuliza kuwa nilichukuliwa vipi hata mimi mwenyewe sielewi, lakini nilishangaa kuona kwamba niko kwenye bonde moja kubwa sana, na lile bonde lilikuwa halina miti wala majani wala ndege na vitu vilivyopo duniani, sehemu yenyewe ilikuwa haivutii hata kidogo, ni sehemu moja iliyokuwa na ukimya wa aina yake. Sasa nikashangaa mbona nilikuwa na rafiki zanguna sasa siwaoni, nikaendelea kujiuliza ni nani aliyenileta huku, na hapa ni wapi? Basi niliamua moyoni mwangu kuwa liwalo na liwe kwa sababu sijui hata aliyenileta mahali hapa, nilikuwa nimekata tamaa, nikajiandaa kutaka kukaa ndipo nikasikia sauti nyumba yangu ikisema Nyisaki nifuate. Nilipoinuka nilishangaa sana kumuona mtu mmoja mfano wa mwanadamu nilipomtazama yule mtu, umbo lake hakuwa mrefu sana wala hakuwa mnene sana, alikuwa ni mtu ambaye sijawahi kumuona popote duniani.Nywele zake zilikuwa ndefu na alikuwa amezibana nyuma kwa banio jekundu, alikuwa amevaa vazi refu mpaka miguuni na jeupe sana ambalo hata weupe wake sijawahi kuuona hapa duniani.Alikuwa ni mweupe sana, siyo weupe wa hapa duniani, macho yake yalikuwa kama mwali wa moto, huyo mtu alikuwa hakanyagi chini bali alikuwa akitembea hewani na vazi lile lilikuwa likingaa sana haliwezi kabisa kutazamika kwa macho ya binadamu. Nayasema mambo ambayo niliagizwa niyaseme, huyu mtu alikuwa amejifunga mkanda mmoja mwekundu kiunoni ndipo nikaamka nikaanza kumfuata. Baada ya hatua chache nikaanza kusikia muungurumo Fulani ambao ulinitisha kwa kiasi Fulani lakini sikuuliza.Kadiri tulivyozidi kutembea mbele ndivyo muungurumo ulivyozidi kuongezeka na kutisha zaidi, mara nikasikia sauti yangu ikiniambia inua macho na tazama mbele, ndipo nikashituka sananilipoona moshi mkubwa mnene na mweusi umefunika bonde lile na kusababisha giza nene katika bonde. Nikamuuliza yule mtu huko mbele kuna nini? Yule mtu akasema, hiyo ni Sehemu ya Jehanamu watakakoenda watenda dhambi baada ya maisha ya duniani Baada ya kusikia hayo yote ndiyo nguvu zikaniishia, nikaanza kulia na kumuomba sana Mungu anisamehe maana kwa mawazo yangu nilifikiri nimekufa na sasa napelekwa Jehanamunikaendelea kulia sana hadi yule mtu aliponieleza usilie maana ukilia utashindwa kuwafikishia watu wangu habari hizi. Hofu ilijia nilitishika mno, lakini mpango wa Mungu kunionyesha mambo haya ni kuwaambia watu. Ndugu msomaji, kweli Jehanamu ninavyoelezwa kuwa ni ziwa la moto elewa hivyo. Nilipotazama sikuona mwisho wake, bali niliona milipuko mikubwa sana na ya kutisha na milipuko hiyo haikufanana na milipuko yoyote hapo duniani labdakwa sehemu inayoweza kulinganishwa na milipuko ya visima vya mafuta.Milipuko hiyo ni mikubwa na inatisha mno iliyosababisha moshi mkubwa sana ulioambatana na moto wa kupaa juu. Moto ule ulijichanganya changanya kama vile bahari iliyochafuka. Kulikuwa na mawimbi makubwa na ya kutisha na yakichanganyika na kutoa miungurumo mikubwa ambayo haiwezi kumfanya mwanadamu kusikia hata mateso ya mwenzake. Mimi nilipokuwa nasikia habari ya Jehanamu nilifikiri labda ni moto mdogo au makaa ya moto. Lakini siku hiyo niliyoona mwenyewe kiasi kwamba nilibaki kulia na kuomboleza kwa uchungu mkubwa mno. Mtu yule alifanya kazi ya kunionya nisilie, pia alinitia nguvu na ndipo nilipoweza kuendelea, ndugu yangu ukisikia Jehanamu iogope kama ulivyo.Nilipoangalia ndani ya ule moto niliona vitu vyenye uhai virefu vyeupe nikauliza hivyo ni vitu gani? Yule mtu akasema hao ni funza wa Jehanamu hizo rangi kwenye pingili zake ni za nini? Akasema hivyo siyo rangi, kama unavyowaona hao funza wana meno hayo manne yenye uwezo hata wa kutoboa fuvu la kichwa cha mtu, na huyo funza akishaingia ndani huacha sumu kali (yahani hiyo unayoiona kama rangi ambayo humtesa mwanadamu milele na milele.Hao funza walikuwa ni wengi sana lakini hawafi ndani ya ule moto, (Marko 9:45-46) walikuwa wembamba warefu yapata mita moja, na walikuwa na pingiri pingiri ambazo zilionekana kuwa na rangi, walikuwa na meno mawili mbele na kichwanikulikuwa na meno mawili jumla ya meno yotemanne, yaani mkiani na kichwani kulikuwa na midomo.Bwana akasema hawafi wala hawaungui kwa sababu wamehifadhiwa kwa ajili ya mateso ya watenda maovu.Ndugu msomaji, nisingeweza kupoteza muda wangu kukuletea jambo ambalo sijaliona lakini nimesema haya ili ukiwa na masikio na uyasikie, ukikataa ni juu yako mwenyewe. Maana sikuambiwa kwamba nimlazimishe mtu aokoke, bali niliambiwa nikamwambie kila mtu labda atakuwepo mmoja atakayegeuka na kuponywa. Sasa nikauliza mbona watu wanasema Jehanamu kuna wanaoungua lakini iweje Jehanamu hii haina watu wanaungua?Akasema wanasema kweli lakini watu watakuja kutupwa kwa wakati wake. Lakini muda huu wamehifadhiwa wakimsubiri baba yao aliyewadanganya (yaani shetani).
Akasema twende nikakuonyeshe nikaanza kumfuata. Kweli ndugu zangu Jehanamu uisikie kama ilivyo. Nilipofikiri habari za wale funza wa ajabu kwa kweli nililia kwa uchungu mkubwa mno nilitetemeka na kuishiwa nguvu nikaanza kuwaza moyoni mwangu mtu anayejua dhambi ni mbaya, na anajua neema ya Mungu na kupuuzia kweli uje kuteswa katika ziwa hili la kutisha lenye moto usiozimika na funza ambao hawafi, kwa kweli nililia sana. Lakini yule mtu akaniambi nyamaza, maana ukilia utashindwa kuyafikisha yote ninayotaka kukuonyesha. Kwa kweli nashindwa hata nieleze vipi. Jehanamu ni kweli ipo na inatisha sana; achana na mafundisho ya mashetani yanayosema hakuna Jehanamu na ukiendelea kufuata hayo utaangamia na kujuta milele. Ninaeleza ndugu yangu kuwa Mungu hapendi upotee ndiyo maana amekupa nafasi kama hii. Nayo yawezekana ni nafasi ya mwisho sasa usipokubali kutubu yawezekana ukajiletea maangamizi wewe mwenyewe.
JEHANAMU IMEANDALIWA KWA AJILI YA SHETANI NA MALAIKA ZAKE
:Niliondoka sehemu hii ya Jehanamu na kuelekea sehemu ya mangojeo nikiwa nalia kwa uchungu mkubwa mno. Na haya ninayokuambia sikutishi bali nakuambia kweli na kama unafikiri nakutisha basi utakwenda kuona mwenyewe.Nikaenda kumfuata yule mtu, tulipofika mahali fulani na kutazama bondeni niliona bonde kubwa lililokuwa limefunikwa giza la kutisha mno. Kabla ya kuwafikia wale watu nilisikia sauti za watu zikilia kwa uchungu mkubwa mno, ndugu yangu kweli Jehanamu kuna vilio vya aina yake, vilio ambavyo huwezi kulia kama walivyokuwa wakilia wale watu, wanalia bila kupumzika. Lile giza nene mno linawafanya wale watu wasiwaze kutazamana kila mmoja na kilio chake na kila mtu na mateso yake hakuna mtu atakayeondoka kwenda kumfariji rafiki yake, kwa sababu kila mmoja aliomboleza kwa ajili ya mateso yake, kadiri tulivyozidi kuteremka lile bonde ndivyo lile giza lilivyozidi kutoweka. Ndipo tulipofika kule bondeni niliona watu wengi mno wasio na idadi; ni wengi kama weusi wa duniani, hakuna mzungu wala mwafrika wote ni weusi kupita kawaida. Na weusi uliosababishwa na baridi kali sana inayopatikana sehemu ile. Na ndimi zao zilikuwa zimevutwa hadi kufikia kila mtu kifuani pake, awe mrefu au mfupi. Nikauliza mbona ndimi zao watu hawa zinafika kifuani? Yule mtu akasema unavyoona sehemu hii haina maji wala haina furaha yoyote, sasa hizo ndimi wanazitumia kwa kulamba machozi, machozi haya hupatikana kwa kilio cha miezi mingi sana kupita na ndipo inatokea chozi moja ambalo hulitumia kama maji.Ndipo nikashikwa na uchungu wa ajabu nikakumbuka hawa ni watu walioishi chini ya Neema ya Mungu, lakini baada ya kufa kwao wako sehemu ya Jehanamu wakimsubiri baba yao aliyewadanganya. Kulikuwa na wanawake na wanaume.Watu wale walikuwa wakilia kwa uchungu mkubwa mno. Nikamwomba yule mtu, nikisema Bwana naomba wachukue watu 100 kutoka kila nchi ili waone hii Jehanamu wawaambie wanadamu watageuka. Akasema wanadamu ni wenye mioyo migumu hata angerudi Yesu mwenyewe wasingemwamini wangeendelea na dhambi. Basi nikaendelea kulia sana. Kisha akaniuliza kama nilikuwa nawafahamu wale watu, nikasema siwafahamu. Akasema twende huku, nikaendelea kukatiza katikati ya mabilioni ya watu waliofia dhambi, kila mmoja na uchungu wake na kila mmoja na mateso yake.Hata wa kwanza kumuona alikuwa Babu yangu mzaa Mama, yeye alikuwa ni Mwinjilisti na Mzee wa Kanisa katika kanisa la Lutherani kule Isapulamo Makete, sasa nilishangaa sana kumuona katika sehemu hii ya Jehanamu, yeye akiwa duniani.alikuwa mweupe sana. Lakini sasa nilishangaa kumuon akiwa mweusi kupita kawaida.Nikamuuliza mbona mtu huyu alikuwa mtumishi wa Mungu na sasa namuona sehemu hii? Yule mtu akasema kweli kabisa huyu mtu alichaguliwa kwa ajili ya kazi ya Mungu lakini aliamua kuifanya kazi ya Mungu na kuingiza michanganyo. Na ndiyo maana ukamuona sehemu hii, ulevi kidogo alikuwa nao, ushurikina kidogo na mambo mengine kama hayo, kama maandiko yasemavyo Ufalme wa Mungu wanauteka wenye nguvu tu. (Matayo 11:12)Mtu wa pili alikuwa jirani yetu, alikuwa ni kaka mmoja aliyekuwa anasali kanisa la Moraviani. Alikuwa ni kaka mmoja aliyejipenda sana na kila siku ya ibada na Jumapili alishika Biblia na kitabu cha nyimbo, kumbe alikuwa hafanyi mapenzi ya Mungu. Hata leo ukienda Uyole utasikia sifa zake. Huyu kaka alikuwa anaumwa sana na amelazwa katika hospitali ya Mbeya, siku mbili kabla ya kufa kwake alituma watu kwenda kumuita mchungaji amwombee na baada ya siku mbili akafa. Sasa nikashangaa sana kumuona sehemu hii ya mateso, wakati huo huo wanasema mtu akiombewa anakwenda moja kwa moja mbinguni? Yule mtu akaniambia kawaambie watu wote duniani, mtu yeyote aliyejua kuwa dhambi ni mbaya na atakwenda Jehanamu, akisema nitatubu, nitatubu nikiona kwamba nimekaribia kufa, mimi huyo simpokei. Jinsi ninyi msivyopokea vitu vilivyooza ndivyo na mimi sivipokei japokuwa navitoa duniani(Ufunuo 22)
Yule kaka akasema ninakuomba kawambie mama, baba na ndugu wasitende dhambi japokuwa mimi nimepata bahati mbaya kuja sehemu hii lakini kawaambie wasitende dhambi.Yule mtu aliyekuwa ananiongoza akasema usiende kuwaambia kwasababu duniani kuna wachungaji na waliookoka wanahubiri Injili wasipowasikia hao, nyumba nzima watakuja huku (Luka 16). Yule kaka akajitupa chini akalia kwa uchungu mkubwa mno.Mtu wa tatu kunionyesha alikuwa Mama yangu mdogo upande wa Mume wangu (Alipokuwa anasafiri mme wake) akakorofishana na wakwe zake ( yaani wazazi wa mume wake) basi akanywa vidonge akafa, mume wake aliporudi na kuonyeswa kaburi mkewe akachukua vidonge akanywa sasa tulipokuwa tunaenda kwa rafiki yetu kumuona ndipo tulipishana na gari iliyokuwa inampeleka hospitali akiwa mahututi. Sasa nikashangaa sana kumuona katika ile sehemu ya mangojeo. Nikauliza huyu mtu niliyemwacha duniani na sasa namuona huku? Yule mtu akasema, kawaambie ndugu zake duniani, mtu anapokufa duniani ile sekunde moja tu, huku amekuwa ameshiriki kiasi cha kutosha, kama ni mtu wa uzima amekuwa na uzima na amekuwa mwenyeji, sasa huyu mtu hapa unavyomwona hata dakika kumi na tano hajamaliza. Nilishangaa sana maana alikuwa mweusi sana, ulimi wake umevutwa na kufika kifuani kama wale wengine. Alionekana kama mtu aliyekaa kwenye mateso yale zaidi ya miaka elfu kumi. Moyo wangu ulijaa huzuni na uchungu usio wa kawaida, basi yule mtu akaniambia sasa kawaambie watu wote jinsi ulivyoona, na jinsi ulivyosikia usiongeze wala usipinguze atakayekataa usimlazimishe wala kumbembeleza, atakayekubari mwongoze sala ya Toba.Ndipo nikashangaa natokea katika nyumba ya yule rafiki yetu, wenzangu wote wametulia wakisubiri litakalotokea basi nikawaeleza yote niliyoyaona na kusikia basi tukamshukuru Mungu.
Comments
Post a Comment