Posts

Showing posts with the label NYISAKI CHAULA PART I

USHUHUDA WA MBINGUNI NA KUZIMU NYISAKI CHAULA

 USHUHUDA WA MBINGUNI NA KUZIMU NYISAKI CHAULA UTANGULIZI:Ndugu yangu kuna shuhuda nyingi sana zinazoanguka duniani, lakini wachache wanaozingatia kwa vile watoaji si wa dini zao au si wa madhehebu yao wala hawajulikani makanisani.Sasa ninakuomba ewe msomaji, tafuta mahali pa utulivu, mwombe Mungu na kusoma ushuhuda huu ili upokee kile ambacho Bwana amekuletea leo. Msichana huyu hivi sasa ameolewa na Mwinjilistii Lemsy Mheni pale Uyole Mbeya kwa lengo la kukuzahuduma yao. Kabila lake ni Mkinga wa Makete,.Msichana huyu anapatikana Uyole njia panda ya Malawi, Zambia na Dar es Salaam pembeni mwa kituo cha mafuta ya magari pale Uyole, Bwana awatangulie katika usomaji. SURA YA 1 KUITWA: Ilikuwa ni mwezi wa 12/1991 tulipochaguliwa vijana 10 kuombea Mkutano wa Kiroho ambao ulikuwa ukifanyika pale Uyole. Siku moja baada ya maombi ya usiku, nilala pamoja na dada zangu. Siku hiyo.nilala usingizi mzito ambao sijapata kuona. Usiku nilishangaa kukuta usingizi umetoweka kabisa,.hivyo nikabaki ni...