Posts

Showing posts with the label NYISAKI CHAULA PART 2

USHUHUDA WA MBINGUNI NA KUZIMU NYISAKI CHAULA

 USHUHUDA WA MBINGUNI NA KUZIMU NYISAKI CHAULA YERUSALEMU MPYA Siku ya tarehe 31/12/1991 niliongozwa na Mama kwenda shambani. Nilimweleza habari zote za baba yake, lakini mama hakuwa na la kufanya zaidi ya kusikitika, kwa maana nafasi ya baba yake ina gharama wala haina budi kuiacha hata milele (Zaburi 49:7-8) Baada kufika shambani nilichimba shimo la kwanza, la pili na tatu kwa ajili ya kupanda mahindi, mara nikaanza kujisikia vibaya, basi nikamwambia mama akasema mwanangu hivi sasa ni saa tatu asubuhi watu wakikuona unarudi nyumbani watashangaa sana, vumilia kidogo. Sasa sikumbuki kama niliongeza kuchimba shimo au hapana. Nilishangaa niko kwenye sehemu nyingine ya tofauti kabisa na mazingira ya dunia, sehemu hii ilikuwa inaleta matumaini sana. Sehemu hii ilinivutia mno basi nikawaza moyoni kama asipotokea yule mtu wa jana nitang'ang'ania huku huku. Nikaamua kukaa mara nikasikia sauti nyuma yangu ikisema tufuate nilipogeuka nikashangaa kuwaona watu wawili waliofanana sana na m...