USHUHUDA WA MBINGUNI NA KUZIMU NYISAKI CHAULA

 USHUHUDA WA MBINGUNI NA KUZIMU

NYISAKI CHAULA

YERUSALEMU MPYA

Siku ya tarehe 31/12/1991 niliongozwa na Mama kwenda shambani. Nilimweleza habari zote za baba yake, lakini mama hakuwa na la kufanya zaidi ya kusikitika, kwa maana nafasi ya baba yake ina gharama wala haina budi kuiacha hata milele (Zaburi 49:7-8) Baada kufika shambani nilichimba shimo la kwanza, la pili na tatu kwa ajili ya kupanda mahindi, mara nikaanza kujisikia vibaya, basi nikamwambia mama akasema mwanangu hivi sasa ni saa tatu asubuhi watu wakikuona unarudi nyumbani watashangaa sana, vumilia kidogo. Sasa sikumbuki kama niliongeza kuchimba shimo au hapana. Nilishangaa niko kwenye sehemu nyingine ya tofauti kabisa na mazingira ya dunia, sehemu hii ilikuwa inaleta matumaini sana. Sehemu hii ilinivutia mno basi nikawaza moyoni kama asipotokea yule mtu wa jana nitang'ang'ania huku huku. Nikaamua kukaa mara nikasikia sauti nyuma yangu ikisema tufuate nilipogeuka nikashangaa kuwaona watu wawili waliofanana sana na mtu wa jana katika hali zote. Mmoja ameshika upanga na alisema anaitwa Mikaeli na aliyekuwa ameshika karatasi alisema anaitwa Gabriel, Wasomaji wa Biblia wanajua kazi zao (Daniel 10:13, Yuda 1:9, Luka 1:26)

Nasikia sauti ndani yangu ikiniambia, inua macho yako utazame mbele nilishangaa sana kuona mbele yetu kulikuwa na nuru kubwa sana kutoka katika mji mmoja mkubwa na mzuri ajabu. Nuru ile iliangaza vizuri kuliko hata mwangaza wa jua na mwezi. Kwa kweli nilivutiwa sana na mji ule jinsi ulivyo na unapendeza. Nikauliza ule mji ni mji gani? Na ni kwa ajili ya nini? Wakaniambia Ule ni mji Mtakatifu, Yerusalem mpya na ni kwa ajili ya Watakatifu walioshinda ya dunia Kwa kweli nashindwa hata kuelezea uzuri wa mji ule maana hauna mfano wa aina yoyote hapa duniani. Tumani langu ni kwenda kuishi katika mji wa utukufu mwingi sijui mwenzangu unatumaini gani? 

Tulipofika mlango wa lile jiji, mawazo yangu yalinipeleka moja kwa moja katika tenzi namba 121 Liko lango moja wazi Niliona lango moja kubwa lililokuwa wazi, (Ufunuo 3:7-8) lango hili lilikuwa likibadirika kila aina ya rangi, nyingine hazipo duniani. Tulipoingia ndani karibu na mlango tulimwona mtu mmoja mzuri sana mweupe na aling'aa sana, alikuwa amekalia kiti kizuri na cha thamani kupita kawaida. Alionekana kuwa mtu mpole mwenye huruma sana na upendo, (Mithali 11:28-30) tabasamu lake lilinipa raha ya aina yake na kuifanya nicheke sana kwa furaha na kujisahau. Malaika nilioongozana nao walianza kuzungumza na yule mtu kwa lugha nisiyoifahamu. Mimi nikaendelea kushangilia ule mji, ule mji umetengenezwa kwa vioo vitupu. Kila sehemu nilipotazama nilijiona mwenyewe (Ufunuo 21:18) nikaendelea kushangilia ule mji kwa uzuri wake na thamani yake hadi pale wale malaika waliponiambia tufuate.

Malaika walinitembeza mji mzima kwa muda mfupi sana hata sekunde moja haikuisha, nilishangaa sana sijui wametembea vipi wale watu. Malaika wa Kwanza akafungua mlango akaingia wa kwanza, pili nikaingia. Katika sehemu hii niliviona viti vingi sana vilivyokuwa vimeandikwa majina kwa damu mbichi. Vile viti vilikuwa vizuri na vya thamani kupita kawaida. Nikaomba kukalia kiti kimoja nikaambiwa utakalia ukishinda ya duniani. Katika sehemu zote sikuona taa zikiangaza lakini kulikuwa na mwanga mzuri sana. Nikauliza mwanga huu unatokana na nini? Akaniambia mwanga huu ni wa mwanakondoo uliyemkuta mlangoni.

Nilipoingia kila mahali niliduwaa kwa kustaajabu ule uzuri wa mji ule. Kila mlango ulibadili baina ya rangi. Tukaondoka sehemu hii. Akafungua mlango mwingine nikastaajabu kuona bustani nzuri sana iliyozungukwa na maua ya majani yote yalikuwa na urefu sawa bila kuzidiana. Tena yalikuwa ya kijani kibichi sana. Maua ya sehemu hii marefu na yanamsifu Mungu kupita kawaida, yakiinama upande wa kulia yanakwenda yote na kusujudu na kuinuka hutoa harufu nzuri sana inayoenea mji mzima, maua hayo yalikuwa yamezungukwa na kioo. Nikasema naomba nichume ua moja nikawaonyeshe ndugu zangu. Akasema maua ya huku hayachumwi, nikasema bustani hii imetengenezwa kwa ajili ya utukufu wa Mungu,nilitamani sana kukaa sehemu hii ya bustani, lakini wakasema tufuate.Kila mahali tulipokwenda mmoja akafuata mwingine, nikasikia sauti nzuri mno zikiimba kwa furaha sana tukaingia, nikashangaa sana kuona watu wengi sana wasio na idadi. Nikajiuliza kwa nini Mungu anasumbuka kuwatafuta wanadamu wakati anao wengi sana? Nikastaajabu sana nikakumbuka pambio moja inayosema; Ukiringaringa kwa Yesu kuna watu wengi. Hawa watu walikuwa wanadamu kama sisi ambao waliishi duniani, lakini wao walimwishia Mungu na kufa na utakatifu.

Kama umewahi kuona mapacha basi wale ni mapacha wa aina yake. Sura zao hazitofautiani hata kidogo wamefanana sana hisivyo kawaida. Nywele zao zilikuwa ndefu wamezibana na banio jekundu sana, wala si wembamba sana na nilifanikiwa kugundua tofauti moja tu. Wengine wamevaa mikanda miwili kiunoni na wengine mkanda mmoja.

Nikauliza kuna tofauti gani kati ya waliovaa mkanda mmoja na waliovaa mikanda miwili? Akasema waliovaa mmoja ni wanaume na waliovaa miwili ni wanawake. Lakini ilikuwa sio rahisi kuwatofautisha kuwa huyu ametoka Taifa hili na yule Taifa lingine, waliimba wimbo mzuri isivyo kawaida, staili za uimbaji wao kwa kweli zilinifurahisha mno, walipunga mikono yao wote kwa pamoja na hapakuwepo hata mmoja wao aliyekosea. Nilipozidi kuwatazama nilitamani sana kujiunga nao ili nami niimbe na kumsifu kama wao wanavyosifu, lakini haikuwezekana kwa sababu hata lugha yao nilikuwa siijui. Baada ya muda akatokea dada mmoja na kuja upande wangu, niliweza kujua ni mwanamke kwa sababu alikuwa na mikanda miwili, nilishangaa kumuona yule dada kwa sababu niliweza kumtambua baada ya sura yake ile ya duniani kutokea. Yeye alikufa mwaka 1987 mwezi wa nne na aliuawa kwa kupigwa risasi.

Yeye alikuwa mwanafunzi wa Shule ya Sekondari (Mbeya Day) kidato cha tatu (Form Three). Aliponifikia alisema Ah Nyisaki, umekuja huku nikasema Ndiyo akasema Za Duniani nikasema Duniani matatizo, akasema Kweli matatizo. Angalia wenzenu tumevikwa miili mipya isiyoharibika, isiyopata magonjwa yaani aliusifu mwili wake na ni kweli ndivyo alivyo (1Korintho 15:40-53) akasema Mwili wa zamani tumeuacha pale, basi nikageuka niangalie amesema wapi, kweli ndugu yangu Biblia inasema mtafuteni Bwana maadamu anapatikana,

mwiteni maadamu yu karibu (Isaya 55:6-7) mambo ya Uyole niliyaona kama vile unavyoweza kutazama kitu kwenye kiganja chako. Nilipoangalia sokoni nikaona biashara zinaendelea kama kawaida, barabarani magari na baiskeli ziliendelea kupishana kama kawaida, nilipotazama makaburini aliponionyesha huyu dada, nikaona makaburi ya watu wengi tena niliweza hata kusoma majina yao. Pia niliweza kujua wazi kabisa kuwa huyu yupo uzimani au jehanamu. Na kama hayupo ilionyesha wazi yuko uzimani. Kaburi la huyu dada lilionekana pia likiwa limepambwa maua. Akasema umekiona kile kitu? Nikasema ndiyo, akasema Ule ni mwili wako. Kwa kweli sikupenda kuutazama mwili mara mbili, mwili wangu niliuona kama ngozi ya kenge chafu sana akaniambia geuka tena, nikakataa, mara ya pili nikakataa, mara ya tatu nikageuka nikaona kama mtu analima na kupanda mbegu akasema yule ni mama yako, fahamu zake tunazo huku, atarudishiwa fahamu utakaporudi wewe. Maono ya siku hiyo yalikuwa ya muda mrefu, kuanzia saa tatu asubuhi hadi saa kumi na mbili jioni. Nilipochukuliwa kwenye maono mama alibeba mwili wangu kuweka kivulini, hapo ndipo nilitambua kweli fahamu zake zilichuliwa. Yule dada akasema Nyisaki kawaambie ndugu zangu wasitende dhambi tena katika mji huu hakuna huzuni, lakini ninawaona wanaendelea na dhambi nasikitika sana, wale Malaika wakasema Usiende kuwaambia kule kuna waliookoka wanahubiri Injili, wasipowasikia hao basi.

Mtu wa pili kunionyesha alikuwa mzee mmoja wa makamo aliyedharauliwa sana pale Uyole, alidharauliwa kwa sababu yeye alikuwa rafiki wa Biblia na Tenzi za Rohoni na kila alipojipumzisha iwe ni shambani, nyumbani au sehemu nyingine yoyote alisoma Biblia, aliimba Tenzi na kuomba, kweli yule alijishusha (Luka 14:35, 18:17, Isaya 51:7- 8) watu walisema amechanganyikiwa. Nilishangaa kumuona katika sehemu hii akiwa kama kijana wa miaka ishirini (20), naye pia aliusifu mwili wake isivyo kawaida, kweli miili ile ni mizuri sana akasema kawaambie wapendwa wa duniani kila mmoja ajitahidi ashinde ya duniani maana muda umeisha, (Ufunuo 22:10-14) kila mmoja aangalie shetani asimpumbaze maana tuna hamu kubwa kuwaona wapendwa wetu, akaondoka akachanganyikana na wenzake. Akatokea mtu wa tatu naye nilimtambua kuwa ni mwanaume kwa sababu ya ule mkanda mmoja, aliponikaribia ikatokea sura ya duniani, yeye alikuwa mzee wa Kipentekoste, alikuwa anasali Kanisa la Assemblies, akasema Ah Chaula umekuja huku nikasema Ndiyo, Za duniani? Duniani matatizo akasema Kweli matatizo, angalieni wenzenu tumevikwa miili mipya isiyosikia njaa, isiyopata magonjwa Basi aliusifu ule mwili, kweli alikuwa amebadilika naye alionekana kama kijana wa miaka ishirini (20) baada ya hapo akaondoka akaendelea kuimba.

Baada ya kuonana na hao watu nikawauliza hao Malaika, hivi hawa watu wanajifunza kuimba?

Wakasema kwa nini unasema hivyo, nikasema wanaimba wimbo hauishi akasema sivyo kama mnavyoimba duniani, maana duniani mkiimba dakika tano mnasema tumemsifu sana Mungu na wengine wanadhani wataenda mbinguni kwa sababu ya uimbaji bila kuokoka. Wimbo mmoja wa huku unaimbwa kwa miezi tisa, beti moja miezi mitatu, Chorus miezi mitatu na beti ya mwisho miezi mitatu, basi nikashangaa sana. Tukaondoka hii sehemu akasema twende nikakuonyeshe watakatifu waliokuwako mwanzo wa kanisa, maana wameletwa sehemu yao akafungua mlango, tukaingia nikaonyeshwa watu kumi na sita (16), lakini nilijua wazi walikuwako na wengine zaidi

Mtu wa kwanza alikuwa Batholomayo, naye akanikumbatia na kunishika mkono, akasema Bwana ndiye aliyechunwa ngozi kwa sababu ya Injili. Na mtu wa pili kunionyesha alikuwa ni

Yohana Mbatizaji, nikasema ndiye aliyekatwa kichwa kwa sababu ya Injili, akasema ndiye huyu.

Basi akanikumbatia na kunishika mkono (Mathayo 14:1-11). Mtu wa tatu kunionyesha alikuwa ni Eliya Mtaabishaji wa Israel (1Wafalme 18:17-18) naye akanikumbatia na kunishika mkono, alinionyesha wengi sana akina Paulo, Petro na Yohana na wengineo.

Batholomayo akasema, Mpendwa, kawaambie wapendwa Duniani, wakaze mwendo maana sekunde moja siyo muda mrefu (Filipi 3:12, 1Korintho 9:24-27), tukaondoka ile sehemu. Wakanipeleka sehemu ambayo zinaandaliwa nguo za kuvaa watakatifu katika karamu ya Mwanakondoo, katika sehemu ile niliwakuta malaika wengi mno wakimsifi Mungu kwa shangwe.

Katika sehemu hii pia kulikuwa na mashine nzuri zilizotengenezwa kwa teknolojia ya hali ya juu mno, nguo nyingi sana ziliingia ndani ya mashine na kutolewa zikiwa zinangaa sana, nikauliza mbona nguo zinatengenezwa nyingi sana, ni za nani?

Maana watu wengi wanakataa wokovu. Akasema Ninyi kaihubiri injili tu, anayetaka kuokoka na aokoke asiyetaka aache, kinachotakiwa ni kwamba anapokuja Mwana wa Adamu asiwepo wa kusema mimi sikusikia. Basi tukaondoka ile sehemu. Ule mji ni sifa kila kinachofanyika, kilifanyika huku wakimsifu Mungu, si malaika wala si mwanadamu, si maua, si vinanda, maana vinanda vya kule vinapiga vyenyewe.Wakanipeleka katika ile sehemu ya awali iliyokuwa na viti vingi vyenye majina yaliyoandikwa kwa damu mbichi.

Tulipofika mara ya kwanza hakukuwa na mtu, lakini muda huu tulimkuta mtu mmoja aliyekuwa akifanya kazi kwa haraka sana, alikuwa amekazana sana kuliko Roboti. Nilimwuliza katika mji huu kuna watu wawili kama hawa? Tena kwa nini wamekazana sana hivi. Akasema huyu ni mtu mmoja kumbuka alipokuwa anaondoka duniani alisema, Ninakwenda kuwaandalia mahali ili alipo nanyi muwepo. (Yohana 14:1-6), akasema huu mji ameuandaa mwenyewe hakuna mtu aliyemsaidia. Tena amekazana kwa sababu muda umefika wa kuchukua walio wake duniani (1Thesalonike 4:13-17). Wakaniondoa sehemu hii. Sehemu inayofuata ni sehemu muhimu sana, umesoma na kusikia zote za kwanza, sasa naomba utulie.

                       MANGOJEO NA JEHANAMU YA PILI:

Mmoja wa wale malaika akaniambia sasa tunakwenda kukuonyesha Jehanamu sehemu ya pili nikasema, Ah kuna sehemu nyingine tena? Akasema Ndiyo, hii imezidishwa ukali mara saba zaidi (Mithali 15:10). Baada ya mazungumzo hayo, ndani yangu furaha ya uzima wa milele ikatoweka nikawaza niwapo sehemu ile nililia vile? Je hii itakuwaje? Nikawafuata katika sehemu hii ya mangojeo peke yake ilinitoa raha, kwa sababu ilikuwa ni kama mara saba zaidi ya ile ya kwanza. Watu wake walitoa sauti za uchungu mkubwa mara saba zaidi, watu niliowaona ni wale wote waliozijua siri za Mungu na kudharau, ni wale wote waliookoka nakuacha wokovu. (Ebrania 2:3, 6:4-6) Ni mchungaji na waalimu (Yakobo 3:1, Ezekieli 34:2-6) wanalia milele na milele bila  kutoa chozi moja. Kabla hata ya kuonyeshwa nililia kwa uchungu sana na kuishiwa nguvu. Akainuka mtu wa kwanza akasema, Bwana naomba umtume mtumishi wako aniletee tone la maji niuburudishe ulimi wangu. Mpendwa hebu jiulize wewe upo duniani, je unaridhika na tone moja la maji? Basi sehemu ile tone la maji lina thamani sana wanalilia tone hilo usiku na mchana. Malaika akawaambia mlipokuwa duniani mliichezea neema ya Mungu, sasa hivi ni sehemu ndogo sana ya mateso bado sehemu yenyewe. Yule mtu akajitupa na kuendelea kulia kwa uchungu mno nilimwangalia tena haikuinuka kabisa.

Nikaendelea kuwafuata wale watu huku nikilia na kutembea kwa taabu mno tukamkuta mtu wa pili akasema, Bwana utupe sekunde 10 tukaihubiri injili ulimwenguni ili waokoke. Yule Malaika akasema mlipokuwa duniani mlikuwa na muda mwingi sana wa kuihubiri injili lakini mliutumia kwa tama zenu sasa hii ni sehemu ndogo tu ya duniani nikalia kwa uchungu sana. Hakuinuka tena, mateso waliyonayo yanawafanya waombe sekunde 10 kuhubiri.Mpendwa muda uliopoteza kwa mambo yasiyo ya maana utadaiwa, maana wewe ungehubiri injili.

Jehanamu ingekosa watu wa kwenda kwa sababu umetumia vizuri muda wako kuhubiri injili. Mara nikasikia kigelegele cha kutisha mno nikauliza hivi, kuna mtu ametupwa motoni? Wakasema hapana. Tumesema jehanamu hii imezidishiwa ukali mara saba zaidi. Sasa kigelegele hicho ni cha moto kikishangilia kwa sababu muda wake umefika. Nikasikia mara nyingine tena, nikauliza vilevile nikaambiwa mbona wewe husikii, jehanamu hii imezidishwa mara saba zaidi. Wale watu wanasikia vigelegele vya kutisha lakini hawana la kufanya zaidi ya kusubiri mateso, tofauti na duniani ambapo mtu akipata shida kidogo anajiua, lakini sehemu hii haiepukiki. Tofauti nyingine tena ni kwamba duniani mtu anayo nafasi ya kutubu, lakini sehemu hii hakuna.Ndani ya ule moto niliwaona FUNZA waliokonda sana, basi nikasikia sauti kutoka upande ule ikisema

Bwana watu uliosema utawaleta watakuja lini? Nikashituka na kuuliza je, huku kuna mtu, funza hao waliongea lugha ya Kiswahili. Akawaambia wale funza subirini kidogo, hapo ndipo walipoonekana kuwa wamechokozwa. Hakukuwa na maelewano kabisa, walipiga kelele wakisema chakula chetu.

Akaniambia hao funza ulivyowaona wamekonda watakapomshika mwanadamu ipo kazi. Nililia sana hadi wale malaika wakaamua kuniondoa sehemu ile; akasema sasa kawaambie watu wote duniani,usiongeze wala usipunguze. Nikasema Bwana mimi duniani siendi wala hapa sikai nipeleke kwa wale wanaoimba. Basi akanigusa bega, nikashangaa natokea shambani saa kumi na mbili jioni na mama ndipo aliposhituka na kuja kuniona.Sasa ndugu yangu, nimekueleza jinsi ilivyokuwa na sasa ni juu yako wewe kuchagua, sikuongeza wala sikupunguza (Mathayo 7:13-14, Kumbukumbu 3:19-20).

MIMI SITAONGEZA NA SASA NI KAZI KWAKO

KUAMUA (Ufunuo 3:20)

MUNGU NA AKUBARIKI.


Comments

DIVINE RELEVATIONS OF HEAVEN AND HELL

DIVINE REVELATION OF WORLDLY APPEARANCE OF WOMEN AND HELL PUNISHMENT BY CHRISTOPHER ZORMELO

MEETING HELD IN THE TERRESTRIAL KINGDOM OF LUCIFER (2) DANIEL GODSWILL

FELLY GRACE OF DR CONGO 3 THE SUN IS COMING DOWN IN JUDGMENT

GODDESS SALONÈ: THE PRINCIPALITY OF HAIR AND BEAUTY SALON ( HAIR RELAXERS, HAIR THREADING AND BLEACHING).

VANESSA CONTROVERSY AT THE GATE OF HEAVEN

SISTER RYE OF IVORY COAST 2 JESUS TOOK ME TO THE UNDERWATER MARINE KINGDOM

LOSING THE CROWN OVER VANITY FELICIANO LIMA OF BRAZIL.

BENJAMIN KIKAMONA THE SEVEN WORLDS OF LUCIFER AFFECTING THE WORLD OF MAN